Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa ameendelea kusimamia mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika uwanja wa Chuo cha Sheria jijini Dar es salaam
Nyota na Katibu Mkuu huyo wa zamani Yanga, amekabidhiwa majukumu wakati kocha mkuu Luc Eymael akisubiriwa kurejea kutoka Ubelgiji
Katika siku ya pili ya mazoezi, Mkwasa ameendelea kuwapa wachezaji wake muda mwingi wa kucheza mpira ili kuhakikisha wanakuwa sawa pale ligi itakaporejea
Juzi alieleza kubaini changamoto ya uzito kwa baadhi ya wachezaji kutokana na kufanya mazoezi magumu bila ya kucheza mpira wakati ligi ilipokuwa imesimama kutokana na corona
Mabingwa hao wa kihistoria wamepania kumaliza msimu kibabe, lengo likiwa kushinda michezo yote iliyobaki ili kukusanya alama 33
Kesho Jumapili, Bodi ya Ligi inatarajiwa kutoa ratiba ya mechi zilizobaki