Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mechi za ligi kuu ya Vodacom pamoja na michuano ya kombe la FA
Kocha Msaidizi Charles Mkwasa ameendelea kusimamia mazoezi hayo wakati Kocha Mkuu Luc Eymael akiwa bado hajarejea
Aidha baada ya mazoezi, wachezaji walipata ugeni wa Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla ambaye aliongozana na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Mhandisi Hersi Said
Ikumbukwe mwishoni mwa wiki hii Yanga itafungua ukurasa mpya kwa kusaini mkataba wa ushirikiano na La Liga katika ufunguzi wa mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa Uendeshaji wa klabu hiyo kongwe zaidi hapa Tanzania





ADVERTISE HERE