Nyota kibao wanaomba usajili Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 May 2020
Nyota kibao wanaomba usajili Yanga

Unaweza kusema huko Jangwani neema inarejea kwa kasi baada ya miaka mitatu ya machozi, jasho na damu..!

Ndio! tangu alipojiuzulu aliyekuwa Mwenyekiti Yusufu Manji ambaye pia alikuwa Mfadhili wa mabingwa hao wa kihistoria, hali ya kiuchumi haikuwa ya kuridhisha

Lakini uongozi wa Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla na ujio wa GSM, ndani ya muda mfupi, umeifanya Yanga iwe timu inayowavutia wachezaji wengi kujiunga nayo

Mwishoni mwa wiki hii mabingwa hao wa kihistoria watasaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya La Liga inayosimamia ligi kuu ya Hispania

Kampuni hiyo imepewa kazi ya kusimamia mchakato wa mabadiliko mfumo wa uendeshaji Yanga, wakitarajiwa kupendekeza mfumo ambao Yanga itautumia

Sasa wakati dirisha la usajili likisubiri kumalizika kwa mechi za viporo ligi kuu, Dk Msolla amefichua kuwa wana orodha ya wachezaji zaidi ya 40 ambao kupitia Mawakala wao, wameomba kusajiliwa na Yanga

"Tuna orodha ndefu ya wachezaji ambao wameomba tuwasajili na wengine Mawakala wao wakileta maombi. Hatutakurupuka kwenye usajili kwani tunafahamu nini tunakitaka kuelekea msimu ujao," alisema Dk Msolla

Aidha Dk Msolla amesema wamejipanga kufanya usajili wa maana na watahakikisha wanamsajili mchezaji yeyote ambaye amependekezwa na kocha Luc Eymael

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’