Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua leo kwenye uwanja wa Chuo cha Sheria jijini Dar es salaam kujiandaa kukamilisha msimu wa ligi kuu ya Vodacom pamoja na michuano ya kombe la FA
Tayari Bodi ya Ligi imetangaza kuwa Ligi itarejea Juni 13 huku droo ya hatua ya robo fainali michuano ya kombe la FA ikitarajiwa kupigwa Ijumaa, May 30 2020
Mazoezi ya mabingwa hao wa kihistoria yanasimamiwa na kocha msaidizi Charles Mkwasa aliyekabidhiwa mikoba baada ya kocha Luc Eymael kushindwa kurejea kwa wakati kutokana na changamoto ya usafiri huko Ubelgiji
Hata hivyo Mbelgiji huyo amekuwa akituma program za mazoezi




ADVERTISE HERE