Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina ambaye yuko nchini Zambia kuhudhuria msiba wa mpwa wake anatarajiwa kurejea Jumatatu ijayo.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amethibitisha kurejea kwa Lwandamina na kukanusha tetesi zinazosambaa kuwa kocha huyo anataka kurudi timu yake ya zamani ya ZESCO.
Ni hivi karibuni Lwandamina ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga na mwenyewe anafurahia changamoto anayoipata katika ligi kuu ya Vodacom.
Baada ya kuiongoza Yanga kutwaa taji la VPL kwa msimu wa tatu mfululizo, Yanga ilianza kwa kusuasua msimu huu kupelekea baadhi ya mashabiki kutaka kocha huyo aondolewe.
Hata hivyo licha ya kukabiliwa na majeruhi mfululizo kwa wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza, Lwandamina ameweza kuirejesha Yanga kwenye kiwango chake na kufufua matumaini ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo.
Tayari timu kadhaa zinazoshiriki VPL zimeelezea kuihofia zaidi Yanga maoni ya hivi karibuni yakiwa ya kocha msaidi wa Simba Masoud DJuma.
Djama, kocha huyo machachari kutoka Rwanda aliishuhudia Yanga kwenye dimba la Taifa katika mchezo dhidi ya timu yake ya Simba na kukiri Yanga ndiyo timu inayoweza kuikosesha Simba ubingwa msimu huu.

ADVERTISE HERE