Yanga kuandika Historia Afrika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 May 2020
Yanga kuandika Historia Afrika

Keshokutwa Jumamosi, May 30 klabu ya Yanga inakwenda kuweka rekodi kwa kuwa timu ya kwanza Barani Afrika kufanya kazi na waendeshaji wa ligi bora duniani, Ligi Kuu ya Hispania, La Liga

Ndio! Mkataba wa makubaliano baina ya Yanga na La Liga utasainiwa Hoteli ya Serena ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga

Yanga wamewaleta La Liga nchini kwa kazi moja tu, kutengeneza mfumo wa uendeshaji ambao utakuwa na tija kwa mabingwa hao wa kihistoria

Shukrani za kipekee ziwaendee kampuni ya GSM, ambao wamedhamini mchakato mzima kuanzia hatua za awali

Kabla ya makubaliano na La Liga, Yanga ilimleta mtaalam kutoka nchini Ureno, Antonio Pinto aliyewahi kufanya kazi katika klabu ya Benfica kwa zaidi ya miaka 10

Hata hivyo mapendekezo yake yalionekana kutokuwa na tija kwa klabu ya Yanga hivyo GSM kuelekea Hispania kufanya mazungumzo na La Liga

La Liga wamefanya kazi na vilabu zaidi ya 40, kwa Afrika Yanga inakuwa klabu ya kwanza

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla anaamini mchakato huo utakapokamilika, Yanga itakuwa mfano na sehemu ya kujifunza kwa vilabu vingine barani Afrika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’