Yanga yajifua Ubungo chini ya Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 May 2020
Yanga yajifua Ubungo chini ya Mkwasa

Kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi leo baada ya miezi miwili ya kukaa nyumbani pasipo kucheza mpira kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona

Mazoezi ya leo yamefanyika uwanja wa Chuo ya Sheria, Ubungo Mawasiliano chini ya kocha msaidizi Charles Mkwasa

Katika siku ya kwanza ya mazoezi, Mkwasa aliwapa wachezaji muda mrefu wa kucheza mpira

Mkwasa ameeleza kuridhishwa na mwenendo wa timu yake lakini amesema wachezaji wake watahitaji muda kuweza kurejea katika ubora wao

"Kimsingi wachezaji wanaonekana kuwa wako fiti, nadhani kila mmoja alikuwa akifanya mazoezi ya nguvu wakati yuko nyumbani"

"Lakini nimeona shida kidogo kwenye umiliki wa mpira, nadhani imechangiwa na wachezaji kufanya mazoezi magumu bila ya kucheza mpira"

"Tutazifanyia kazi changamoto tulizoziona ili kuhakikisha tunakuwa sawa kabla ya ligi kurejea," amesema Mkwasa

Yanga ina viporo vya michezo 11 pale ligi itakaporejea. Wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia alama 51

 

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’