Eymael ampa 'tano' Mkwasa kuiongoza Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 May 2020
Eymael ampa 'tano' Mkwasa kuiongoza Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema hana wasiwasi kikosi chake kuwa chini ya kocha Msaidizi Charles Mkwasa kwani anamuamini

Eymael amekwama nchini Ubelgiji akikabiliwa na changamoto ya usafiri kurejea nchini ambapo amebainisha kuwa anaweza kusafiri Juni 01

Uongozi wa Yanga umemkabidhi majukumu ya kuiongoza timu Mkwasa ili kuhakikisha kikosi kinakuwa tayari pale ligi itakaporejea

"Sina tatizo kabisa kwa Mkwasa kukabidhiwa timu. Nafahamu ni kocha mwenye uzoefu mkubwa na nitajitahidi kushirikiana nae pamoja na kuwa bado niko hapa Ubelgiji, " alisema Eymael

Aidha Eymael amesema kuwa anasubiri uongozi wa Yanga kukamilisha taratibu za safari yake lakini anaweza kuondoka Ubelgiji May 31 na ndege ambayo inasafiri moja kwa moja kuja Tanzania

"Nasubiri taratibu zikamilishwe na Yanga lakini ningependa nisafiri na ndege ambayo itatua Tanzania Juni mosi"

Mbelgiji huyo amesema timu yake inahitaji kufanya vizuri katika mechi zilizobaki akiitizama zaidi michuano ya kombe la FA ambayo inaweza kuwapa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao

Kikosi cha Yanga kinaanza mazoezi leo kujiandaa na mikiki mikiki hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’