Wakati Ligi Kuu ya Vodacom ikitarajiwa kurejea muda wowote, mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere anapewa nafasi ya kuifikia rekodi ya mabao ndani ya msimu mmoja iliyowekwa na Mohammed Hussein 'Mmachinga' miaka ya 90 wakati akiitumikia Yanga
Mmachinga aliweka kambani mabao 26 na kuweka rekodi hiyo ambayo mpaka sasa ni Abdallah Juma wa Mtibwa Sugar aliyekaribia kuivunja mwanzoni mwa miaka ya 2000 baada ya kufunga mabao 25
Mmachinga aliweka rekodi hiyo wakati huo ligi kuu ikishirikisha timu 12 kwa maana ni katika michezo 22 tu
Hivyo hata ikitokea kwa Kagere ambaye mpaka sasa amefunga mabao 19 ktika mechi 28 na mechi zikiwa zimebaki 10, akifunga mabao 26 au zaidi haiwezi kushindanishwa na rekodi ya Mmachinga ambayo aliiweka kati michezo 22 tu
Lakini upekee mwingine wa rekodi ya Mmachinga, unatokana na kuwa mabao yake yote alifunga bila ya msaada wa mikwaju ya penati
Kwa maana katika mabao yote 26 aliyofunga, hakuna bao hata moja alilofunga kwa mkwaju wa penati
Mmachinga anabaki kuwa mmoja wa washambuliaji hatari watakaobaki kwenye historia ya soka la Tanzania kutokana na umahiri wake katika kuzifumania nyavu