Mwili wa Mwalusako kuzikwa Kyela

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 May 2020
Mwili wa Mwalusako kuzikwa Kyela

Mwili wa aliyewahi kuwa Katibu na Mchezaji wa zamani wa Yanga Lawrence Mwalusako utasafirishwa Siku ya Jumatano 27/05/2020 kwenda Kyela Mjini kwa mazishi siku ya Alhamis 28/05/2020

Mwalusako alifariki leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha nyota huyo wa zamani wa timu ya Taifa

"Tumepokea kwa mshtuko taarifa ya kifo cha mpendwa wetu, kama uongozi wa klabu tunasema tumempoteza mtu muhimu ambaye kwa muda wote tangu akipojiunga na Yanga kama mchezaji na baadaye kuwa Kiongozi alikuwa mstari wa mbele kupigania maslahi na maendeleo ya klabu yetu," amesema Katibu Mkuu wa Yanga Dkt. David Ruhago.

"Tutashiriki kikamilifu kwenye msiba huu wa Mwalusako ambaye enzi za uchezaji wake alikuwa Beki mahiri aliyemudu kucheza nafasi zote za ulinzi"

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu, Kimara Jijini Dar es Salaam

Marehemu Laurence Mwalusako alichezea Yanga na Taifa Stars miaka ya 1980, na baadae alikuwa Katibu Mkuu wa Yanga mwaka 2013

Alisajiliwa Yanga mwaka 1985 akitokea Pan Africans na tangu hapo ameendelea kuwa Mwanayanga hadi mwisho wa uhai wake.

Haikuwa dunia ila ni mapito Bwana katoa na bwana katwaa jina lake lihimidiwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’