Kulingana na taarifa iliyotolewa na Katibu wa Kamati ya Mashindano Yanga, Deo Mutta, siku ya Jumanne saa kumi jioni wachezaji wote wa Yanga wataripoti Uwanja wa Mazoezi kwa ajili ya Vipimo mbalimbali kama Uzito, Covid19, Malaria, Glucometer-Kupima Sukari Mwilini na maelekezo mbalimbali jinsi ya kujikinga na Covid19.
Aidha, Yanga imemualika Dr Marealle Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya Tiba CAF na Mjumbe wa Kamati ya Tiba TFF kutoa darasa kwa ufupi kwa wachezaji kuhusu Covid 19.
Siku hiyo Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla na Wadhamini wa klabu hiyo watapata wasaa wa kuzungumza na wachezaji kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo michezo iliyobaki.
Hakutakuwa na ruhusa kwa mtu yeyote asiyehusika kuingia uwanjani kwenye mazoezi ya timu kwa ajili ya uzingativu wa Maelekezo ya Serikali