Baada ya kufanya mazoezi binafsi kwa takribani miezi miwili, beki Alli Mtoni Sonso amesema yuko tayari kurejea katika mazoezi ya pamoja na wachezaji wengine
Mtoni ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliotumia ipasavyo muda wa kufanya mazoezi wenyewe tangu ligi iliposimama kutokana na changamoto ya corona March 17
Beki huyo kiraka amesema anasubiri zoezi la kupimwa uzito ambalo wachezaji wote wa Yanga watakumbana nalo pale watakaporudi kambini Jumanne
Kwa wachezaji ambao watakutwa na uzito mkubwa huenda wakakumbana na adhabu ikiwa ni pamoja na kukatwa mshahara!, Mtoni anaamini adhabu hiyo haitamkumba
Mshike mshike wa Ligi Kuu unatarajiwa kurejea Juni 01, kwa ajili ya kumalizia mechi 93 zilizobaki ili kukamilisha msimu
Yanga ina viporo vya michezo 11