Tutamaliza msimu kwa heshima - Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 May 2020
Tutamaliza msimu kwa heshima - Eymael

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema wamepania kumaliza msimu kwa heshima ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

Eymael yuko kwenye mchakato wa kurejea nchini. Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema tayari wamechukua hatua kuhakikisha kocha huyo anarejea mapema licha ya changamoto ya usafiri inayomkabili huko Ubelgiji

Mbelgiji huyo amesema pamoja na kuwa na nafasi finyu ya kutwaa ubingwa, amesema watahakikisha angalau wamalize nafasi ya pili huku akipigia hesabu michuano ya FA

"Haitakuwa rahisi kuishusha Simba katika nafasi ya kwanza lakini nina imani kubwa kuwa tunaweza kufanya vizuri hata angalau kumaliza katika nafasi ya pili. Tutaanza kufanya mazoezi pamoja, tutaangalia utimamu wa miili ya wachezaji wetu ambao walikuwa wakifanya mazoezi peke yao"

"Tunahitaji kumaliza msimu kwa kishindo, ni lengo letu kuhakikisha tunapata nafasi ya kushirki michuano ya Kimataifa msimu ujao, tutahitaji kushinda taji la FA," alisema

Aidha Eymael ameeleza kufurahishwa na uamuzi wa Serikali kuamua mechi zote za ligi kuu na kombe la FA zipigwe jijini Dar es salaam

Eymael ni miongoni mwa makocha waliotoa mapendekezo akishauri mechi hizo zichezwe katika kituo kimoja hasa Dar es salaam kutokana na mji huo kuwa na miundombinu ya kutosha

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’