Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuanza mazoezi keshokutwa baada ya sikukuu ya Eid El Fitri chini ya kocha msaidizi Charles Mkwasa
Mkwasa ataongoza mazoezi hayo wakati uongozi ukiendelea na mchakato wa kuwarejesha nchini Kocha Mkuu Luc Eymael ambaye yuko Ubelgiji na kocha wa viungo Riedoh Berdien
Akizungumza mapema jana, Mkwasa alisema maandalizi ya kuanza program za mazoezi yamekamilika na watakuwa uwanjani baada ya sikukuu ya Eid
"Maandalizi yamekamilika, uwanja uko tayari kinachosubiriwa kwa sasa ni kumalizika kwa sikukuu ya Eid na Mwongozo wa Afya wa TFF, Bodi ya Ligi na Serikali," alisema
"Kabla ya kuanza mazoezi, tutawapima Afya wachezaji wote chini ya Madaktari wetu, na vipimo vingine ambavyo vitatolewa na TFF pamoja na Serikali"
"Tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mechi zilizobaki ili tuweze kumaliza ligi tukiwa katika nafasi nzuri"
Β