Tangu mwezi Januari Yanga ilikuwa ikihusishwa kumuwania beki wa kushoto wa Rayon Sports na timu ya Taifa ya Rwanda Erick Rutanga
Nyota huyo ilibaki kidogo tu atue Jangwani usajili wa dirisha dogo kabla ya dili lake kukwama dakika za majeruhi
Sasa taarifa za uhakika ni kuwa huenda mwamba huyo ataitumikia Yanga msimu ujao baada ya GSM, moja ya wadhamini wa mabingwa hao wa kihistoria kumalizana nae pamoja na klabu yake ya Rayon
Inafahamika, nafasi ya beki wa kushoto ni miongoni mwa nafasi zilizopewa kipaumbele na kocha Luc Eymael katika usajili wa kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao
GSM wamepania kwelikweli kutengeneza kikosi cha maangamizi ambacho msimu ujao hakuna kingine zaidi ya kuutaka ubingwa wa 28 ligi kuu ya Vodacom
ADVERTISE HERE