Taarifa imeripotiwa kwenye baadhi ya Magazeti ni kuwa Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amepanga kumleta mshambuliaji Andrea Fileccia kutoka nchini Ubelgiji
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amewahi kufanya kazi na Eymael nchini Afrika Kusini
Kwa sasa Fileccia anakipiga katika Klabu ya Royal Francs Borains ya nchini Ubelgiji
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa klabu ya Yanga kusajili mchezaji mzungu kama dili hilo litafanikiwa
Miaka michache iliyopita Yanga ilisajili Wabrazil watatu lakini kabla iliwahi kumsajili kipa mzungu Obren Curkovic
ADVERTISE HERE