Baada ya Rais Dk John Magufuli kuruhusu michezo kuanzia Juni Mosi, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi wanasubiriwa kutoa utaratibu na ratiba ya mechi zilizosalia
Ratiba ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) nayo inasubiriwa kwa hamu pia
Yanga imejipanga kumaliza kwa kishindo ligi lakini kipaumbele zaidi ni dhahiri kitakuwa kwenye FA
Ubingwa wa FA utaihakikishia Yanga kushiriki michuano ya CAF Confederation msimu ujao
Inaelezwa droo ya hatua ya robo fainali itafanyika karibuni ikiwa ni pamoja na utaratibu wa jinsi mechi za hatua hiyo zitakavyopigwa
Awali mchezo wa fainali ulipangwa kuchezwa kule Rukwa lakini yanaweza kutokea mabadiliko hasa kama mechi zitarejeshwa bila ya mashabiki
Mapendekezo yaliyotolewa na wadau ni mechi zote kupigwa katika kituo kimoja