Yanga inahesabu siku tu kabla ya kusaini mkataba na La Liga kusimamia mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo
Inaelezwa Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambaye kampuni yake inasimamia mchakato huo, yuko nchini Hispania kuweka mambo sawa
Jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Hersi alibandika picha akiwa na Mkuu wa LaLiga Global Network Juan Botella huko Hispania
Taarifa za ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa Mkataba rasmi wa ushirikiano na La Liga utasainiwa kabla ya mwezi huu kumalizika
ADVERTISE HERE