Wakati wa Rais wa nchi Dk John Magufuli akitangaza ruhusa michezo iliyokuwa imesitishwa kutokana na janga la corona kurejeshwa kuanzia Juni Mosi, uongozi wa klabu ya Yanga umeanza taratibu za kuwarejesha makocha wake Luc Eymael (Kocha Mkuu) na Riedoh Berdien (kocha wa viungo)
Eymael yuko Ubelgiji ambako alikwenda kufunga ndoa kabla ya kukutana na vikwazo vya usafiri vilivyosababishwa na corona na hivyo kushindwa kurejea nchini tangu mwezi March
Beldien yeye alirejea kwao Afrika Kusini
Afisa Habari wa Yanga Hassani Bumbuli amesema tayari wameanza taratibu za kuwarejesha makocha hao ili kuhakikisha wanawahi kusimamia majukumu yao katika ngwe ya lala salama
"Tumepanga kuwakatia tiketi baada ya Rais kutangaza kuwa ndeg kutoka mataifa mengine zitaanza kuruhusiwa, kwa hiyo tunaangalia ndege gani itamfaa na kocha wetu anaweza kurejea ndani ya siku tatu (3) zijazo ili kuwa tayari kwa maandalizi," amesema
Aidha, kwa upande wa mlinda lango Farouk Shikhalo, Bumbuli amesema klabu ya Yanga itafanya juhudi zote kuhakikisha anarejea kwa wakati licha ya Kenya kufunga mipaka ya baadhi ya mikoa yake