Kessy asisitiza dhamira ya ubingwa haijapotea Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
9 Nov 2017
Kessy asisitiza dhamira ya ubingwa haijapotea Yanga
Beki wa kulia wa Yanga, Hassan Ramadhani ‘Kessy’ amesema kwamba pamoja na changamoto zinazowakabili kwa sasa, lakini dhamira inabaki pale pale, kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Katika mahojiano maalumu na mtandao wa Bin Zubeiry Sports , Kessy amesema kwamba Ligi Kuu bado ipo katika hatua za awali mno, hivyo ni mapema kuanza kubashiri bingwa.

Kessy amesema hadi sasa mwenendo wa Yanga si mbaya kwenye Ligi Kuu, isipokuwa tu msimu huu unaonekana utakuwa na ushindani zaidi.

Amesema timu zilizoibuka na ushindi katika raundi ya tisa zinaweza kukwama katika raundi ijayo, wakati zilizokwama raundi iliyopita zinaweza kuibuka raundi ya 10.

“Ndiyo hivyo, yaani kuna timu unacheza nayo hata wewe mwenyewe ukipata sare unashukuru, lakini kuna timu nyingine ukitoka nayo sare unajilaumu. Singida ni kati ya timu ngumu msimu huu zimesajili vizuri na zina motisha nzuri kwa wachezaji wake na hamasa kubwa,”amesema.

Yanga inaendelea na mazoezi mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu, baada ya Jumamosi ya wiki iliyopita kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Singiza United Uwanja wa Namfua, Singida.

Mabingwa hao mara tatu mfululizo, wanatarajiwa kuteremka tena dimbani, Novemba 19 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kumenyana na Mbeya City.

Kwa sasa Yanga inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu kwa pointi zake 17, baada ya kucheza mechi tisa, ikiwa nyuma ya Simba na Azam FC zenye pointi 19 kila mmoja baada ya kucheza mechi tisa pia.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →