Kampuni ya La Liga imethibitisha kuwa watakuja nchini kuongoza mchakato wa Mabadiliko mfumo wa uendeshaji klabu ya Yanga
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema wakati wowote watampokea Mwakilishi wa kampuni hiyo ambaye atashirikiana na Kamati Ndogo ya Mabadiliko iliyoundwa na Yanga
"Ni tukio la kipekee na la kusisimua, tunasubiri kwa hamu kuanza mchakato huo," ulisomeka ujumbe wa La Liga waliotuma kwenye ukurasa wa Instagram wa klabu ya Yanga
Yanga itakuwa klabu ya kwanza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kupata nafasi ya kufanya kazi na kampuni kubwa inayosimamia moja ya ligi bora zaidi duniani, La Liga
Wanayanga wametakiwa kuwa pamoja kumuunga mkono Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla pamoja na timu yake ambayo imedhamiria kukamilisha mchakato huo ambao unakwenda kuifanya Yanga iendeshwe katika mfumo wa kipekee