Uongozi wa klabu ya Yanga umejipanga kufanya kampeni kubwa kutoa elimu kwa Wanachama na Mashabiki wake wakae tayari kupokea mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo
Jana Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alizindua kampeni hiyo yenye kauli mbiu ya TWENZETU KWENYE MABADILIKO
Msemaji na Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema wamejipanga kuendesha kampeni babkubwa kupitia Azam TV na Mitandao ya kijamii kuwapa elimu Wanayanga wote lengo likiwa kuweka msimamo mmoja kuelekea jambo hilo kubwa
Kampuni ya GSM ambayo ni moja ya wadhamini wa klabu ya Yanga, wamejitolea kusimamia mchakato mzima ikiwa ni pamoja na kugharamia mahitaji yote kuanzia masuala ya kampeni
GSM ndio waliofanikisha makubaliano na La Liga kusimamia mchakato huo ambapo wakati wowote tukio la kusainiwa mkataba kati ya Yanga na La Liga litafanyika na huo ndo utakuwa ukurasa mpya wa muelekeo wa Yanga
Nugaz amesema wamewachagua La Liga kwa sababu wana uzoefu mkubwa na usimamizi wa michakato hiyo wakiwa wamehusika kuzitengenezea mifumo timu 42
"Tuungane pamoja Wanayanga wote, tumshike Mwenyekiti wetu Dk Mshindo Msolla na tuwape ushirikiano Kamati ndogo iliyoundwa kusimamia mchakato ambayo iko chini ya Mwanasheria Msomi Alex Mgongolwa, twendeni sote kwenye Mabadiliko," ametamba Nugaz