Nyota Fc Lupopo afichua mpango wa kutua Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 May 2020
Nyota Fc Lupopo afichua mpango wa kutua Yanga

Mshambuliaji wa Fc Lupopo Mpiana Monzizi amefichua kuwa anasubiri kumalizika changamoto ya corona ili aweze kuja nchini kujiunga na mabingwa wa kihistoria, Yanga

Monzizi aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya DR Congo akifungana na Jackson Muleka na Fiston Mayeke wa AS Vita wote wakifunga mabao 12

Hivi karibuni nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi alifichua uwezekano wa Yanga kumsajili mshambuliaji huyo ambaye pia ni raia wa DR Congo

Mshambuliaji huyo amenukuliwa na gazeti Mwanaspoti akithibitisha kufanya mazungumzo na Yanga huku akibainisha kuwa kilichobaki ni kwake kusaini mkataba

"Tulishazungumza kila kitu na kufikia makubaliano, Kilichobaki ni kumalizana ili tujue msimu ujao tunauanzaje," amesema

"Tunasubiri ndege zianze kutembea pengine baada ya hii corona naweza kuja Tanzania kusaini mkataba"

"Nimekuwa nikizungumza mara kwa mara na Tshishimbi akiniambia mambo mengi kuhusu ligi ya Tanzania. Sioni kama nitashindwa kufanya vizuri"

Monzizi ni miongoni mwa washambuliaji Wacongomani ambao wanatajwa kuwaniwa na Yanga

Wengine ni Heritier Makambo na winga Tusila Kisinda ambaye naye inaelezwa dili lake limefika pazuri

DR Congo imemaliza msimu kwa kuwapa ubingwa TP Mazembe ambao walikuwa wakiongoza ligi kwa tofauti ya alama 12 ligi iliposimama miezi miwili iliyopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
51m ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’