Makocha kupewa nafasi kuziandaa timu zao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2020
Makocha kupewa nafasi kuziandaa timu zao

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo amesema makocha wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu wasiwe na wasiwasi kwani watapewa muda wa kuziandaa timu zao kabla ya ligi kurejea

Baada ya Rais Dk John Magufuli jana kutangaza kuwa anafikiria kuruhusu shughuli za michezo wiki hii, wadau wa soka wamekuwa na shauku kusikia ni lini ligi hiyo itarajea

"Kwa sasa tunaendelea na maandalizi, kwa kiasi kikubwa tuko tayari, kinachosubiriwa ni ruhusa ya Serikali tu. Tutazipa timu muda wa kufanya maandalizi kabla ya mechi kuanza kuchezwa. Hatuwezi kuanza moja kwa moja tu, hivyo niwatoe hofu makocha, watakuwa na nafasi ya kuandaa timu zao," amesema Kasongo

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto amesema tayari wameanza kulipa madeni ya Waamuzi baada ya kupokea fedha za FIFA

Mguto amesema wamejipanga kumalizia ngwe iliyobaki kuhitimisha msimu wanachosubiri ni tuhusa ya Serikali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’