Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesisitiza kuwa Shirikisho lake halikupokea fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kwa ajili ya michuano ya AFCON 2019 ngazi ya vijana umri chini ya miaka 17 ambayo ilifanyika nchini
Karia amesema fedha hizo zilienda Wizarani lakini pia amesema ni vyema TAKUKURU wanachunguza sakata hilo na watawapa ushirikiano wote watakaotaka kutoka kwao
"Tulipewa zile pesa na zikaenda Wizarani, kwa kweli tunamshukuru Rais kwa msaada wake mkubwa ambao uliwezesha michuano ile kufanyika. Tulikuwa na hali mbaya sana ya kiuchumi," Karia aliliambia shirika la Utangazaji TBC
"Pesa ilienda Baraza la Michezo, TFF hatukupokea pesa na hata Katibu Mkuu ambaye ndiye anahusika na masuala ya akaunti pia alisema hakupokea"
"Mimi kama Rais wa TFF nafurahi hili jambo kwenda TAKUKURU, nimetukanwa sana pamoja na kusemwa hivyo tuwaachie TAKUKURU wafanye kazi yao"
Karia aliongeza kuwa mchango wa Rais Magufuli na Serikali kwa kiasi kikubwa uliwezesha kufanyika vyema kwa mashindano hayo ingawa bado kuna madeni yaliyosalia