Mashabiki waliniondoa Yanga - Balinya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 May 2020
Mashabiki waliniondoa Yanga - Balinya

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Juma Balinya amesema sababu kubwa iliyomfanya aondoke katika kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria ni kutokubalika kwa mashabiki

Balinya aliomba mkataba wake uvunjwe na Yanga mwezi Januari baada ya kushindwa kutamba

Hata hivyo nyota huyo raia wa Uganda amefichua kuwa hakuwa na furaha pale alipoona hapewi sapoti na mashabiki wakati alipokuwa hafanyi vizuri

"Nilitamani kuendelea kubaki Yanga licha ya changamoto zilizokuwepo lakini sikuweza kwani mashabiki hawakunikubali"

"Mchezaji ni rafiki wa mashabiki kama, hawakubali kazi yako huwezi kujisikia faraja," alisema Balinya

Baada ya kuachana na Yanga, Balinya alisajiliwa na klabu ya Gor Mahia ambapo alifanikiwa kufunga mabao mawili katika mchezo wake wa kwanza ligi kuu ya Kenya

Mpaka ligi inasimama kutokana na janga la corona huko Kenya, Balinya alikuwa amefunga mabao matatu

Hata hivyo Kenya tayari wamefuta msimu wakiitangaza Gor kuwa mabingwa wakitumia sheria yao ya dharura

Balinya amesema yuko mbioni kuondoka Gor Mahia akiwa amepata ofa kutoka klabu ya Polokwane inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini

Gor Mahia inakabiliwa na changamoto ya ukata, wachezaji wengi wakidai mishahara ya hadi miezi minne

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’