Nyota wapya Yanga kufanyiwa tathmini kitaalamu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 May 2020
Nyota wapya Yanga kufanyiwa tathmini kitaalamu

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amefichua kuwa utaratibu watakaotumia kufanya usajili utawawezesha kunasa wachezaji bora

Shauku kubwa ya mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao inarejesha ufalme wake kwenye soka la Tanzania huu ukiwa ni msimu wa tatu bila ya kushinda taji

Aidha wachezaji wengi waliosajiliwa katika kipindi hicho, hawakukidhi ubora na mahitaji ya timu jambo lililopelekea wengine kuvunjiwa mikataba

Eymael amesema watafanya usajili wa kisasa kwa kutumia Wataalam ambao wamewapa kazi ya kufuatilia wachezaji

"Tunashirikiana na kampuni za wataalam kutoka Afrika Kusini ambao wanatusaidia kufuatilia kila mchezaji tunayetaka kumsajili. Hawa wanazo taarifa sahihi kuhusu wachezaji wengi Afrika, taarifa ambazo zitatusaidia katika kufanya maamuzi," amesema

"Utaona tunahusishwa na wachezaji wengi, lakini nikuhakikishie tutasajili wachezaji sahihi kulingana na ubora wao ili tuwe na timu yenye kuweza kushinda ubingwa msimu ujao," amesema

Matumizi ya makampuni katika kufanya 'scouting' ya wachezaji ni njia sahihi ya kupata wachezaji wazuri sokoni

Pamoja na utaratibu huo kuwa na gharama, lakini mwisho wa siku klabu hunufaika kwa kusajili wachezaji ambao wana uhakika na uwezo wao

Usajili holela wakati mwingine huziingiza timu gharama mfano hai ukiwa klabu ya Yanga ambayo mwezi Januari ililazimika kuvunja mikataba ya wachezaji watano ambao hawakukidhi viwango

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’