Inaelezwa beki wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto ambaye mazungumzo ya usajili wake kuelekea Yanga yanaendelea, ametaka kitita cha Tsh Milioni 100 ili aweze kumwaga wino Jangwani
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Coastal Union Hussein Ally aliuambia mtandao wa daboten kwamba Yanga ndio klabu pekee hadi sasa iliyofika kwenye uongozi wa klabu hiyo ili kukamilisha usajili wa Mwamnyeto
Hata hivyo kumeibuka sintofahamu baada ya mchezaji kukataa dau alilowekewa mezani ambalo ni Tsh Milioni 60
Ally amesema Mwamyeto ametaka kititaΒ cha Tsh Miloni 100, jambo ambalo Yanga hawakukubaliana nalo
Awali ilitaarifiwa kuwa mwishoni mwa wiki hii Mwamnyeto, Yanga, Coastal Union na GSM walitarajiwa kukutana kukamilisha dili la usajili wa nyota huyo
Hata hivyo kama ataendelea kushikilia msimamo wa kutaka Tsh Milioni 100 huenda Yanga wakasitisha mpango wao wa kumsajili