Hoja muhimu mjadala wa idadi ya nyota wa kigeni

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
13 May 2020
Hoja muhimu mjadala wa idadi ya nyota wa kigeni

Mchambuzi mahiri wa soka nchini Edo Kumwembe anasema hoja ya kupunguza nyota wa kigeni kwenye ligi zetu haina mashiko kwa kuwa hata idadi ya wageni ni wachache sana ukilinganisha na wazawa

Lakini pamoja na wazawa kuwa wengi, bado ukiangalia timu zinazofanya vizuri ni zile zenye wachezaji wengi wa kigeni

Kwa maana rahisi ni kuwa kama utapunguza idadi ya nyota wa kigeni katika vilabu vyetu, pia tutashusha viwango vya baadhi ya timu ambazo zinamudu gharama ya kuwa na idadi ya nyota wa kigeni waliopendekezwa

Hapa hoja ya msingi sio kupunguza idadi ya nyota wa kigeni bali ni kuinua viwango vya wachezaji wazawa kwa kutengeneza program nzuri za soka zitakazowasadia kuinuka

Jitihada zinazofanywa sasa na TFF za kuvitaka vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu kuwa na timu za vijana U17 na U20, inafaa zitiliwe mkazo kwani miaka michache baadae faida yake inaweza kuonekana

Lakini pia suala la viwanja nalo liangaliwe kwa jicho tofauti. Kumekuwa na uhaba wa viwanja bora vya soka hapa nchini. Suala la kutengeneza wachezaji wazuri linahitaji miundombinu mizuri ya viwanja

Kama nchi hatuwezi kupiga hatua kwenye soka kama tutaendelea kuwa na viwanja ambavyo havina viwango vinavyotakikana

Pamoja na changamoto iliyopo, nyota wengi wa kigeni wanaokuja kucheza hapa nchini wanakuwa wameiva kulinganisha na wachezaji wazawa wengi

Mkazo zaidi unaweza kuwekwa kwenye utaratibu wa kuwapata nyota hao, tunaweza kuongeza masharti kwa wachezaji wanaosajiliwa bila ya kupunguza idadi

Mfano ni pendekezo lililotolewa la kutaka wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa hapa nchini wawe wanacheza timu za Mataifa yao

Wachezaji wa aina hii wengi wanakuwa bora hivyo hata gharama za kuwapata zinakuwa ziko juu

Ukiwa na sheria kama hiyo ni vilabu vyenyewe vitakavyoamua ni wachezaji wangapi wanaweza kuwasajili na pengine idadi inaweza kuwa hata chini ya hao 10 waliopo sasa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
51m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’