Kiungo mshambuliaji wa Yanga Deus Kaseke ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inafika tamati msimu huu utakapomalizika
Nyota huyo ambaye alisajiliwa na Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2015, anawasikilizia mabosi wake ofa ya mkataba mpya
Hata hivyo amesema pamoja na kuwasilizia Yanga, yuko tayari kusikiliza ofa kutoka timu nyingine ambazo zinahitaji huduma yake
"Bado nina mkataba na Yanga mpaka mwishoni mwa msimu, nasubiri ofa ya mkataba mpya. Kipaumbele nimeipa Yanga lakini hata ikitokea timu nyingine tukafikia makubaliano, sina pingamizi," amesema
Kaseke amekuwa na vipindi tofauti kwenye kikosi cha Yanga
Mpaka wakati ligi inasimama, Kaseke hakuwa na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Luc Eymael
Inafahamika Yanga iko kwenye mkakati kabambe wa kukisuka upya kikosi chake ambapo nafasi ya washambuliaji wa pembeni ikipewa kipaumbele
Eymael ndiye atakayeamua kama nyota huyo apewe mkataba au la