Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela amependekeza mechi zilizobaki kupigwa kwenye kituo kimoja ili kuharakisha kumaliza msimu
Kiongozi huyo amesema jiji la Dar es salaam linaweza kuwa sehemu sahihi kwa mechi zote kupigwa na kumalizika kwa wakati bila ya kuathiri maandalizi ya msimu ujao
"Kwa muda uliobaki, TFF na Bodi ya ligi wanapaswa kuja na utaratibu ambao utawezesha ligi kumalizika kwa haraka ili kuanza maandalizi ya msimu ujao"
"Tukitumia utaratibu wa kawaida kuna hatari ligi inaweza kwenda mpaka mwezi wa nane. Hapo timu hazijafanya usajili wala maandalizi ya msimu mwingine"
"Wanaweza kuchagua mkoa wa Dar es salaam kuwa kituo cha mechi zote kuchezwa. Vipo viwanja vya kutosha Azam Complex, Uwanja wa Taifa, Uhuru na hata uwanja wa Karume ambapo mechi hata nne zinaweza kuchezwa kwa siku"
"Dar inao uwezo wa kupokea timu zote 20 muhimu ni kuandaa taratibu za kiusalama kuhakikisha taratibu zote za kujikinga na corona zinazingatiwa," amesema