Mohammed Issa 'Banka' kiungo mkabaji wa Mtibwa Sugar tayari ameanza kuangaliwa kwa karibu na vigogo wa soka nchini zikiwemo Simba na Yanga.
Naweza kusema huyu ndiye 'Tshishimbi' wa Mtibwa Sugar. Katika robo ya kwanza ya msimu huu amekuwa masaada mkubwa kwa timu yake ambayo ina alama 17 sawa na Yanga.
Uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi fupi, ndefu kadhalika kutengeneza nafasi za kufunga unamtofautisha na viungo wengi wazawa.
Natamani sana Yanga ifanye jitihada za kumnasa kwenye dirisha dogo la usajili kwani huyu akitua Yanga safu ya kiungo itakuwa imeshiba hasa.
Wakati wote ambao Kamusoko ni majeruhi Yanga imekuwa ikimtegemea Tshishimbi zaidi kwenye sehemu ya kiungo akisaidiana na Pato Ngonyani/Raphael Daudi.
Tshishimbi amedhihirisha kuwa akichezeshwa kiungo cha juu ni hatari zaidi. Kwenye mchezo dhidi ya Simba tuliona uwezo wake wa kupiga mashuti na kutengeneza nafasi za kufunga.
Mohammed Issa, Thabani Kamusoko na Tshishimbi inaweza kuwa safu bora zaidi ya kiungo ambayo itakuwa na mafanikio kwa Yanga.
Ni muhimu Yanga kuimarisha kikosi chake hasa ikizingatiwa katika mzunguuko wa pili wa VPL itakabiliwa na michuano zaidi kama kombe la FA (ASFC) na ligi ya mabingwa.

ADVERTISE HERE