Eymael alivyobadili maisha ya Makapu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 May 2020
Eymael alivyobadili maisha ya Makapu

Kabla ya ujio wa kocha Luc Eymael kiungo kiraka Said Juma Makapu hakuwa akionekana kama ni mchezaji ambaye angeendelea kudumu Yanga kwa muda mrefu

Msimu uliopita aliongezwa mkataba wa mwaka mmoja, tena ilikuwa wakati dirisha la usajili likielekea ukingoni

Yeye na Jaffar Mohammed ni wachezaji ambao walipewa mikataba dakika za mwisho

Ukizungumzia wachezaji ambao wamekaa Yanga kwa muda mrefu, Makapu ni miongoni mwa wachezaji hao kwani alisajiliwa na Yanga tangu enzi za kocha Marcio Mexime

Kabla ya Eymael, Makapu amepita mikononi mwa Maximo, Hans van Pluijm, George Lwandamina na Mwinyi Zahera

Katika makocha wote, hakuna hata mmoja ambaye alimuhakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza

Lakini ujio wa Eymael umekuwa na mafanikio kwake kwani ni kocha aliyeonekana kumuamini tangu alipomuona mazoezini kwa mara ya kwanza

Eymael akambadilishia majukumu kwam kurudisha kwenye nafasi ya ulinzi ambayo amekuwa akicheza ingawa sio kila mara

Kwa sasa Makapu ni mmoja wa wachezaji ambao hawana wasiwasi na maisha yao Yanga kwani anao uhakika wa kupata mkataba mpya

Makapu amesema imani aliyopewa na Eymael ilimfanya yeye mwenyewe ajiamini na kujituma zaidi ili kuhakikisha hamuangushi Mbelgiji huyo ambaye alikiri kuona kitu tofauti kutoka kwa beki huyo mstaarabu

"Namshukuru sana kocha (Eymael) amenisaidia sana, amenifanya nijiamini zaidi na kuweza kucheza kwa uhuru. Nafahamu bado sijafika ninapotaka lakini kwa usaidizi wake na ushirikiano na wachezaji wenzangu, nitaendelea kusonga mbele," amesema

Kiwango alichoonyesha Makapu tangu alipoanza kutumiwa na Eymael nafasi ya ulinzi, kilimfanya ajumuishwe kwenye kikosi cha timu ya Taifa ambacho kilipaswa kushiriki michuano ya CHAN ambayo hata hivyo haikufanyika kutokana na janga la corona

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’