Beki kiraka wa Yanga Said Juma Makapu amesema kabla ya ligi kurejea, ni vyema timu zikapewa muda wa kutosha kujiandaa ili kuweza kurejesha ushindani waliokuwa nao wakati ligi iliposimama
Wachezaji wamekuwa majumbani tangu March 17 baada ya Serikali kusimamisha shughuli zote za michezo kudhibiti maambukizi ya virusi vvya COVID-19
Makapu amesema kwa kuwa wamekaa muda mrefu bila ya kucheza mpira, ameshauri ni vyema TFF wakatoa muda kwa timu kufanya maandalizi
"Tunahitaji hata kucheza mechi za kirafiki ili tuweze kurejesha miili katika ushindani tukiokuwa nao mwanzo. Kurejea uwanjani bila kupata muda wa kutosha kujiandaa kunaweza kuna na athari ya ligi kukosa ushindani kwa kuwa wachezaji hawatakuwa sawa," amesema
Kwa sasa wachezaji wameendelea kufanya mazoezi kwa kujisimamia wenyewe licha ya makocha kuwapa program za mazoezi hayo
Upo uwezekano TFF itavipa vilabu angalau wiki mbili za kufanya mazoezi ya pamoja kabla ya kurejea kwa ligi