Niyonzima ajichimbia ufukweni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 May 2020
Niyonzima ajichimbia ufukweni

Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amesema wakati huu ligi ikiwa imesimama, anaendelea kujiweka sawa tayari kwa kuisaidia timu yake pale ligi itakaporejea

Pamoja na kutekeleza program ya mazoezi ya timu, nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda amesema kila siku jioni hufanya mazoezi ufukweni akijumuika na wachezaji wa timu mbalimbali

"Kwa kawaida asubuhi tunafanya mazoezi ya timu, jioni najumuika na wachezaji wa timu nyingine kufanya mazoezi hapa ufukweni"

"Tunafanya mazoezi mchanganyiko ikiwa ni pamoja na kukimbia, kucheza mpira muhimu kujinga stamina na kuongeza pumzi ili wakati ligi itakaporejea tuwe sawasawa," amesema Niyonzima

Niyonzima amekuwa na mwanzo mzuri katika awamu yake ya pili kunako klabu ya Yanga aliyojiunga nayo mwezi Januari 2020

Kwa mara ya kwanza Niyonzima alisajiliwa na Yanga mwaka 2012, akacheza kwa misimu mitano kisha kujiunga na Simba mwaka 2017 ambako alicheza kwa misimu miwili

Alirejea Yanga akitokea klabu ya AS Kigali ya kwao Rwanda ambayo aliitumikia kwa miezi sita tu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’