Wakati mkataba wake na Yanga ukitarajiwa kumalizika mwakani, uongozi wa timu hiyo uko mbioni kumuongeza mkataba beki wake kisiki, Lamine Moro
Moro alitua Yanga mwaka jana akitokea klabu ya Buildcon ya nchini Zambia
Tangu ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria, amekuwa nguzo ya safu ya ulinzi
Moro raia wa Ghana amebainisha kuwa tayari ameanza mazungumzo na mabosi wake ili aweze kuongeza mkataba
Amesema hafikirii kuondoka Yanga ndio maana yuko tayari kusaini mkataba utakaomuweka Jangwani kwa muda mrefu
Nyota huyo ataungana na Maproo wengine Bernard Morrison na Papy Tshishimbi ambayo tayari wamesaini mikataba mipya kuendelea kukipiga Jangwani
ADVERTISE HERE