Mkwasa kuiongoza Yanga Eymael akichelewa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 May 2020
Mkwasa kuiongoza Yanga Eymael akichelewa

Kama ligi itarejea mapema klabu ya Yanga huenda ikakosa huduma ya kocha wake Luc Eymael ambaye bado amekwama Ubelgiji kutokana na changamoto za usafiri zilizosababishwa na ugonjwa wa corona

Hata hivyo hilo haliwezi kuwa tatizo kwani mabingwa hao wa kihistoria wanae kocha wao msaidizi Charles Mkwasa ambaye alikuwa akiinoa timu hiyo kabla ya Eymael kutua mwezi Januari

Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema hakutakuwa na changamoto yoyote kama ikitokea Eymael atachelewa kurudi nchini kwa kuwa yupo Mkwasa

"Ligi hata ikirejea kesho timu itakuwa chini ya kocha Mkwasa na hakutakuwa na tofauti yoyote kwakua ana uwezo mkubwa na ana uzoefu huku akiifahamu vizuri Yanga hivyo hakutakuwa na upungufu kwenye benchi la ufundi," alisema Nugaz

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli alidokeza kuwa anafikiria kuruhusu ligi kuendelea baada ya kushauriana na wataalam wake wa afya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’