Wakati huu ligi ikiwa imesimama kutokana na janga la corona, wachezaji wa Yanga wameendelea kujifua kujiweka tayari kwa mapambano pale ligi itakaporejea
Beki Andrew Vicent Chikupe maarufu kama Dante ni mmoja wa wachezaji wanaotumia kipindi hiki kujiweka sawa
Tangu arejeshwe kikosini mwezi Januari, beki huyo kisiki hajaweza kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza pengine kutokana na ushindani wa namba uliopo katika nafasi ya ulinzi anayocheza
Chikupe amebainisha kuwa amejipanga kupigania nafasi yake pale ligi itakaporejea
Nyota huyo ameweka bayana mpango wake ni kuhakikisha anarudi katika nafasi yake
Mkataba wake na Yanga unafikia tamati mwishoni mwa msimu hivyo ligi itakaporejea itakuwa nafasi kwake kuwashawishi mabosi wake wampe mkataba mpya