Uongozi wa klabu ya Yanga uko mbioni kusaini mkataba wa ushirikiano na Bodi ya uendeshaji ligi kuu ya Hispania, La Liga
Mabingwa hao wa kihistoria, wanakwenda kuweka historia nyingine kubwa kwa kusaini mkataba na Bodi inayoendesha moja ya ligi bora duniani, La Liga
Wadhamini wa klabu ya Yanga, GSM wamehusika kwa kiasi kikubwa kuwezesha mpango huu ambao pia utashuhudia Yanga ikiingia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji
Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama wa Yanga, Simon Patrick amethibitisha kuwa tayari wamemaliza kuupitia mkataba huo na sasa wanawasubri La Liga waweke hadharani tarehe ya mkataba huo kusainiwa
Ikumbukwe Yanga pia itaingia makubaliano ya ushirikiano na moja ya klabu kongwe inayoshiriki ligi kuu ya Hispania, makubaliano ambayo yataishuhudia Yanga ikiweza kupata uzoefu na mbinu za uendeshaji wa kisasa
Kupitia dili hilo, inaelezwa Yanga itakuwa na ushirikiano wa moja kwa moja wa kitimu, mbinu na hata vifaa vya mazoezi
Kwa hakika klabu ya Yanga imejipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kiuendeshaji na pengine itakuwa somo kwa vilabu vingi barani Afrika