Mwamnyeto aomba ushauri wa Baba wapi akacheze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2020
Mwamnyeto aomba ushauri wa Baba wapi akacheze

Inaelezwa klabu ya Yanga iko kwenye nafasi nzuri ya kuinasa saini ya beki wa kati wa Coastal Union Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye siku za karibuni tetesi za usajili kumuhusu zimetawala kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti ya michezo nchini

Klabu za Yanga na Simba zinatajwa kuchuana vikali kumnasa beki huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye pia hucheza timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Yanga inatajwa kutoa ofa nono zaidi kuliko wapinzani wake na kilichokuwa kikisubiriwa ni makubaliano na mchezaji mwenyewe

Kabla ya kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria, Mwamnyeto aliomba apewe mudaΒ  azungumze na baba yake mzazi, Mzee Nondo Mwamnyeto baada ya kutokea sintofahamu baina ya Mawakala wake

Mzee Mwamnyeto amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti akithibitisha kuzungumza na Wanawe na kumshauri achague timu ambayo imempa maslahi mazuri

"Nimemuita na nimezungumza nae. Nimemwambia sawa mimi ni baba yake lakini uamuzi wa mwisho kuhusu wapi atakwenda kucheza atauchukua mwenyewe"

"Kuna mambo mengi ya kuangalia kuna maslahi na ubora wa klabu anayotaka sasa. Hivyo atakapoona kuna sehemu imempa maslahi mazuri basi asaini tu wala asisubiri uamuzi wangu," amesema Mzee Nondo

Je usajili wa Mwamnyeto Yanga ataweza kuwapa changamoto walinzi waliopo kwenye kikosi cha Yanga sasa?

Walinzi wanaotumika zaidi na kocha Luc Eymael ni Lamine Moro, Kelvin Yondani, Ally Mtoni na Said Juma Makapu

Lakini pia wapo Andrew Vicent na Ally Ally

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’