Mshambuliaji wa Kagera Sugar Kelvin Sabato amemtaja mshambuliaji wa Yanga David Molinga ni miongoni mwa washambuliaji anaowakubali lakini hajapewa nafasi ya kuonyesha makali yake
Sabato amesema Molinga ni mchezaji mwenye vitu vingi mguuni lakini pengine wachezaji anaocheza nao Yanga hawajui jinsi ya kumtumia
Sabato amesema mshambuliaji yeyote anahitaji kutengenezewa nafasi ili aweze kufunga, hivyo kama hapati nafasi ni wazi ataonekana hafai
"Mimi kwangu Molinga ni bonge la mshambuliaji. Kama mchezaji na mdau wa soka ambaye nafuatilia mambo, nimebaini jamaa ana vitu vikubwa sana mguuni"
"Kama mshambuliaji ili niweze kun'gara ninategemea sana nafasi ninazotengenezewa na watu waliokuwa nyuma yangu, je waliokuwa nyuma yake wanamtengenezea nafasi?, " Sabato aliiambia EA radio

Molinga ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga akiwa ametupia mabao nane, msimu huu
Mcongomani huyo amesema anaweza kufunga mabao zaidi ligi itakaporejea kama atapewa nafasi na kocha Luc Eymael
Mkataba wake na Yanga unamalizika mwezi August na kumekuwa na tetesi kuwa mabingwa hao wa kihistoria huenda hawatampa mkataba mpya