Eymael apania kuimarisha safu ya ulinzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 May 2020
Eymael apania kuimarisha safu ya ulinzi

Aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisajili idadi kubwa ya wachezaji kwenye nafasi ya ulinzi, hasa walinzi wa kati, lakini kocha wa sasa Luc Eymael amependekeza usajili wa mlinzi mwingine wa kati

Walinzi waliosajiliwa wakati wa Zahera ni Lamine Moro, Mustafa Selemani, Ally Mtoni na Ally Ally na wakati huohuo Yanga ikiwa na Kelvin Yondani na Andrew Vicent ambaye alirejeshwa kikosini baada ya GSM kumaliza sakata lake la madai dhidi ya uongozi wa Yanga

Mustafa yeye mkataba wake ulivunjwa mwezi Januari wakati Ally Ally alitolewa kwa mkopo lakini akagoma kwa kuwa timu aliyopelekwa sio timu ambayo mwenyewe alipendekeza

Kati ya walinzi waliopo, Eymael ameonekana kumkubali zaidi Lamine Moro huku akieleza kuridhishwa na uwezo wa mkongwe Yondani ambaye hata hivyo makali yake yanapungua kutokana na umri wake unazidi kumtupa mkono. Ifikapo Oktoba 09 Yondani atakuwa na miaka 36

Mbelgiji huyo alilazimika kumtumia Said Juma Makapu nafasi ya mlinzi wa kati ambapo kwa kiasi kikubwa alifanya vizuri kuliko wengi walivyotarajia

Eymael anataka mlinzi mwingine wa kati ambaye atashirikiana na Lamine, Makapu, Mtoni na pengine Yondani kwa kuwa Chikupe huenda asiwe sehemu ya kikosi cha Yanga pale mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu

Tangu Eymael alipotua Yanga mwezi Januari, Chikupe hakuwahi kupata nafasi ya kucheza. Mchezo pekee aliocheza tangu arejee Yanga baada ya mgogoro wake kumalizika ni mchezo wa kwanza dhidi ya Simba ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2

Mlinzi na nahodha wa Nkana Fc, ambaye pia hucheza timu ya Taifa ya Kenya Mussa Mohammed alifichua kuwa kwenye mazungumzo na mabosi wa Yanga ambao wanataka huduma yake

Lakini pia inaelezwa Yanga inakaribia kumnasa mlinzi wa Coastal Union, Bakari Nondo Mwamnyeto ikielezwa kuwa mazungumzo baina ya Yanga na Coastal yamefika pazuri na kilichokuwa kinasubiriwa ni makubaliano binafsi na mchezaji

Kama Yanga itafanikiwa kumpata mmoja au hata walinzi wote, Eymael atakuwa amemaliza changamoto kwenye safu yake ya ulinzi ambayo msimu huu imeruhusu mabao 20 huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 31 tu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’