Beki wa Yanga Ally Mtoni 'Sonso' amesema wako tayari kwa uamuzi wowote utakaochukuliwa kuhusu kurejea kwa ligi kuu ya Vodacom
Juzi Rais wa nchi Dk John Magufuli aliondoa sintofahamu iliyokuwepo kuhusu hatma ya ligi baada ya kubainisha kuwa anafikiria kuruhusu ligi hiyo iendelee licha ya uwepo wa ugonjwa wa corona
Rais Magufuli alisema uamuzi huo ukatekelezwa baada ya kushauriana na wataalamu wake wa Afya
Mtoni ambaye hivi karibuni aliachana na ukapera baada ya kufunga ndoa, amesema yeye binafsi yuko tayari kuendeleza pale alipoishia ligi iliposimamishwa March 17
"Mimi niko tayari kwa uamuzi wowote wa Serikali. Nimekuwa nikifanya mazoezi kujiweka sawa hivyo sina wasiwasi," amesema
Wadau wa soka nchini wamepokea kwa furaha kauli ya Rais Magufuli kuhusu kurejea kwa ligi kwani wamekosa burudani kwa takribani siku 49
Hata hivyo uamuzi wa mwisho wa lini ligi itarejea utatolewa na Serikali ambapo jana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilivitaka vilabu kuendelea na utaratibu uliotangazwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kijikinga na maambukizi ya corona
TFF imesisitiza hakuna ruhusa iliyotolewa kufanya mikusanyiko hivyo vilabu haziruhusiwi kurejea mazoezini mpaka pale watakapoelekezwa kufanya hivyo