Katika kipindi cha miaka 10, takwimu zinaibeba klabu ya Yanga kuwa timu iliyofanikiwa zaidi kuliko timu nyingine yoyote Tanzania
Ndio! Pamoja na kuukosa ubingwa wa ligi kuu kwa misimu miwili mfululizo, Yanga bado inashikilia rekodi ya kushinda mataji mengi katika kipindi hicho
Tangu mwaka 2010, Yanga imeshinda mataji matano ya ligi, mataji mawili ya michuano ya CECAFA(Kagame Cup) na taji moja la kombe la Shirikisho la Azam
Kwa mikakati iliyopangwa huko Jangwani, ni wazi mabingwa hao wa kihistoria msimu ujao wamepania kuanza upya hesabu ya mataji kwa muongo mwingine
Kwa ubingwa wa ligi kuu Yanga bado inaongoza kwa mbaali dhidi ya watani zao Simba, wakiweka kibindoni mataji 27
Ni nadra sana kwa Yanga kukaa zaidi ya misimu mitatu bila ya kushinda taji lolote
Changamoto za kiuchumi zilizowakabili wababe hao wa soka la Tanzania katika kipindi cha miaka minne iliyopita, zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya kushinda mataji
Lakini ujio wa GSM ni dhahiri utakuwa na kishindo kikubwa msimu ujao