Mkufunzi wa klabu ya Yanga Luc Eymael amepongeza uamuzi wa Rais wa Tanzania Dk John Magufuli kuruhusu ligi kuu ya Vodacom kuendelea siku za usoni
Eymael amekuwa mstari wa mbele akitoa maoni kwa TFF na Bodi ya Ligi wahakikishe mechi zilizosalia zinacheza ili kila timu ipate haki yake
Mbelgiji huyo amesema ni jukumu la Bodi ya Ligi kuhakikisha wanaandaa utaratibu ambao utawezesha mechi zilizobaki zinachezwa katika mazingira salama ambapo mashabiki wanapaswa kushudia michezo hiyo kupitia runinga zao majumbani
Aidha, Eymael ameshauri kuwa ni vyema mechi hizo zikapigwa kwenye kituo kimoja kuliko utaratibu wa timu kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine
"Ligi yetu ina wachezaji 600, hivyo tunaweza kupima jumla ya watu 1,500 ambao hawa ndio wakawa wahusika wa moja kwa wa mechi zote, ikawa rahisi, kwa kweli mimi napenda sana soka lichezwe na ligi imalizike tuangalie mambo mengine ya msimu ujao," Eymael amenukuliwa na mtandao rasmi wa klabu ya Yanga
Eymael bado yuko Ubelgiji ambako amekwama kutokana na mashirika mengi ya ndege kusitisha safari za Kimataifa, changamoto ya ugonjwa wa corona
Β