Ligi ikirejea mechi zitapigwa nyumbani na ugenini kama kawaida

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2020
Ligi ikirejea mechi zitapigwa nyumbani na ugenini kama kawaida

Bodi ya Ligi kuu (TPLB) imetoa mapendekezo ya ligi kuu ya Vodacom, Ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili kurejea mwezi Juni lakini uamuzi huo ukisubiri ruhusa ya Serikali kutegemeana mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini

Pamoja na wadau wengi kupendekeza mechi kupigwa katika vituo maalum badala ya timu kusafiri mikoani, Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Almas Kasongo amesema watatumia utaratibu wa kawaida kwa timu kucheza nyumbani na ugenini

"Baada ya kikao chetu cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika mwishoni mwa wiki, tumekubaliana kama Serikali itaturuhusu, ligi irejee mwezi Juni ambapo tutahakikisha mechi zinachezwa kwenye mazingira salama zaidi"

"Tumeridhia utaratibu wa zamani wa mechi kuchezwa nyumbani na ugenini utumike lakini tutakuwa makini kuhakikisha wachezaji, waamuzi, makocha, viongozi na wandishi wa habari ambao wataruhusiwa kuingia uwanjani wanafanyiwa vipimo"

Kasongo amesema idadi ya mechi ambazo zimebaki, mechi 98 ligi kuu, mechi 48 ligi daraja la kwanza na mzunguuko mmoja pamoja na mechi 10 za play-off ligi daraja la pili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’