Ukizungumzia wapiga mipira mahiri ya adhabu kwenye ligi kuu ya Vodacom msimu huu, huwezi kukosa kutaja jina la mshambuliaji wa Yanga David Molinga 'Falcao'
Katika mabao nane aliyofunga kwenye ligi, mabao matatu yalitokana na mipira iliyokufa
Nyota huyo amefichua kuwa ufundi wa kupiga mipira hiyo alijifunza kutoka kwa kiungo wa zamani wa klabu za manchester United na Real Madrid, David Beckham
Molinga ameeleza kuwa alikuwa akivutiwa sana na umahiri wa Beckham kwenye kupiga mipira ya adhabu
"Nisema ukweli, nimejifunza kupiga mipira ya adhabu kutoka kwa Beckham. Kwa kiasi kikubwa nami magoli yangu mengi nafunga kupitia mipira hiyo. Enzi za Beckham inapotokea adhabu karibu na lango wengi walihesabu ni goli kwani mapigo yake ilikuwa sawa na mkwaju wa penati," amesema
Molinga aliyetua Yanga msimu huu akitokea ligi ya Congo, amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kocha Luc Eymael licha ya kuwa ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga
Amesema kama atapewa nafasi mara kwa mara kwenye mechi zilizosalia, anaouwezo wa kufunga mabao sita au zaidi
Molinga amejiwekea malengo ya kumaliza msimu akiwa amefunga angalau mabao 15