Mshambuliaji wa Kagera Sugar Yusufu Mhilu amesema yuko tayari kurejea klabu ya Yanga kama atapewa ofa nono
Mhilu ni miongoni mwa vinara wa kutupia mabao msimu huu akiwa ameifungia Kagera Sugar mabao 11 kwenye ligi kuu ya Vodacom
Anashika nafasi ya pili katika orodha ya vinara wa mabao, akiwa sawa na Reliants Lusajo wa Namungo Fc
Mshambuliaji huyo aliyelelewa na Yanga tangu timu ya vijana, yuko ukiongoni mwa mkataba wake wa mwaka mmoja aliosaini kunako klabu ya Kagera Sugar mwanzoni mwa msimu
Amesema bado hajapokea ofa rasmi kutoka kwa viongozi wa Yanga licha ya kusikia tetesi ya kutakiwa na mabosi wake hao wa zamani
Lakini kama viongozi watamfuata, amesema atakuwa tayari kurejea makubaliano yakifikiwa
ADVERTISE HERE