Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kupokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mdau mkubwa wa maendeleo ya soka nchini Dk Maneno Tamba ambaye alifariki dunia mapema leo na amezikwa jioni ya leo jijini Dar es salaam
Dk Tamba alikuwa Mwanachama wa Yanga ambapo mpaka umauti unamfika mapema leo, alikuwa Mjumbe wa timu ya Wanawake Yanga Princess, Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Dar es Salaam na mmiliki wa klabu ya Mburahati Queens

ADVERTISE HERE