Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison amesema kuwa ana shauku kubwa ya ligi kurejea aendelee majukumu yake ya kuwapa furaha mashabiki
Ligi imesimama kwa zaidi ya siku 40, Serikali ikichukua uamuzi wa kusimamisha shughuli zote za michezo zinazohusisha mikusanyiko ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona
Morrison alishuka dimbani kwa mara ya mwisho March 15 kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao ulipigwa Ruangwa,mkoani Lindi
Mghana huyo aliyejizolea sifa kemkem kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchezea mpira, amesema anakumbuka sana shamrashamra na shangwe la mashabiki pale walipofunga


"Nimekumbuka zile shamrashamra za kushangilia bao tunapokuwa tumefunga, au nimefunga mimi au kumsaidia mwenzangu kwa namna yoyote ile afunge bao na mwisho wa siku litufanye kuibuka washindi.
"Hali hiyo kiukweli nimekuwa nikiikumbuka kiasi kwamba natamani ligi ianze hata leo ili mradi tu niweze kuendelea na majukumu yangu yaliyonileta hapa nchini ya kuisaidia Yanga kupata ushindi," alisema
Nyota huyo ameendelea kufanya mazoezi binafsi kujiweka sawa tayari kwa hatua zozote ambazo zitachukuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) pale mambo yatakapokuwa sawa
Hata hivyo bado haijafahamika kama ligi itarejea au msimu utafutwa kutokana na mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona nchini